Comments

Friday, 5 June 2015

PEPONI DUNIANI (19/10/10)


Wametuvisha miwani,

Miwani ya juani,

Kutupeleka peponi,
Peponi duniani.

Mbona sasa hatuoni?

Hatuoni yalo mbeleni,
Giza limo machoni,
Macho yamo gizani.


Miwani ya jua gizani?!

Gizani tusiwabaini,
Wamebeba vitu pomoni,
Pomoni bila sisi baini.


Tumepumbazwa akili,

Akili zikakubali,
Tukavikwa na bangili,
Bangili lisilo fahali.

Sasa nchi I mashakani,

Mashakani kwa madeni,
Na wananchi wa vitani,
Vita vya umasikini.


Hatujafika peponi,

Peponi ku duniani,
Tumejiweka motoni,
Motoni limo shetani.
By: Finland Bernard

0 comments:

Post a Comment